Zephaniah 2:4-7

Dhidi Ya Ufilisti


4 aGaza utaachwa
na Ashkeloni utaachwa magofu.
Wakati wa adhuhuri Ashdodi utaachwa mtupu
na Ekroni utang’olewa.

5 bOle wenu ninyi ambao mnaishi kando ya bahari,
enyi Wakerethi;
neno la Bwana liko dhidi yenu,
ee Kanaani, nchi ya Wafilisti.

“Mimi nitawaangamiza,
na hakuna atakayebaki.”


6 cNchi kando ya bahari, mahali ambapo wanaishi Wakerethi,
patakuwa mahali pa wachungaji
na mazizi ya kondoo.

7 dItakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda,
hapo watapata malisho.
Wakati wa jioni watajilaza chini
katika nyumba za Ashkeloni.
Bwana Mwenyezi Mungu wao atawatunza,
naye atawarudishia wafungwa wao.
Copyright information for SwhKC